Ukiongea na mtoto mdogo atakuambia anatamani kuwa mkubwa na kuanza kujitegemea, sawa sawa na mtu alie Advance anavyotamani kwenda chuo bila kuwaza ya kwamba tunavyokuwa majukumu nayo yanaongezeka. Ila ndo ‘nature’ yetu wanadamu, kuwa na expectations ya mazuri tu bila kuziwazia changamoto tunazotakiwa kuzipitia ili kufikia hizo expectation zetu
2013 ndio mwaka nilikutana na Salim ila sio kwa ukaribu kwani ndio mwaka tulianza kusoma shule mmoja. Tulipokaribia kuhitimu kidato cha nne ndipo ukaribu wangu na salim ulijengeka na ilitokana na kuwa tulijikuta wote tunataka kubadilisha ‘curriculum’ na ndipo tukawa tunakaa Pamoja na kuapply shule Pamoja. Na hio safari ya urafiki ndipo ilianzia hapo na nikabahatika kumaliza nae mpaka chuo kimmoja tukiwa tunafanya course mmoja. Ingawa ndio mtu ambaye nabisha nae sana, Salim ni kati ya watu ninao wajua ambao ni humble sana na mshauri mzurii sana.
Kwenye episode hii Salim amejaribu kutupa experience yake ya kielimu alioipata sehem tofauti. Kajaribu pia kutoa maoni yake juu ya education system iliopo Tanzania kulingana na exposure yake alioipata kwa kupata nafasi yakusoma UK pia. Humu ndani pia tumeongelea vitu vya ku concider kabla ya kuchagua chuo na mafunzo machache aliyoyapata salim, kutokana na chuo.
Funzo kubwa nilioipata kupitia epidode hii ni kuwa tuwe tunafikiria jambo kwa ukubwa sana kabla ya kufanya na tukiwa tunafikiria tuwe tunaziangalia pande zote mbili za shilingi na tusiangalie upande mmoja tu.
01/11/23 • 37 min
Generate a badge
Get a badge for your website that links back to this episode
<a href="https://goodpods.com/podcasts/the-insightful-podcast-show-tips-214721/the-story-time-what-to-expect-while-in-uni-27340036"> <img src="https://storage.googleapis.com/goodpods-images-bucket/badges/generic-badge-1.svg" alt="listen to the story time: what to expect while in uni on goodpods" style="width: 225px" /> </a>
Copy